Uhali gani mpenzi msomaji, wa blog hii na leo katika uwanja huu wa viatu tutazungumzia
aina ya viatu vya wazi pia tuta changanua mambo mengi kuhusu aina hii ikiwemo
wakati gani wa kuvi vaa, mazingira, na jinsi ya kuilinda miguu yako ili isi
chafuke unapo vaa viatu vya aina hii.
Viatu hivi upendezea sanasana kuvaliwa wakati wa
masika kwa sababu viatu vinafanya miguu yako isitoe harufu mbaya kwa sababu
wakati wa mvua ukiwa umevaa viatu vya kufunika maji yanapo ingia kwenye kiatu
chako yanaweza kukusababishia miguu kutoa harufu mbaya mda wote au kukuletea
fangasi kwa sababu ya ule unyevu unyevu uliopo katika viatu vyako.
Vilevile kuna baadhi ya watu ambao awapendelei kuvaa viatu
vya wazi kwa sababu akitembea hatua mbili au tatu unakuta amesha chafuka lakini
pia kuna watu ata atembee navyo kuanzia hasubui mpaka jioni
miguu yake bado inaonekana kuwa misafi.
Viatu vya wazi ni vizuri sana vinafanya miguu yako iwe na
muonekano mzuri na inakuepushia sugu katika miguu yako ukiwa unavaa mara kwa
mara ni tofauti na viatu vya kufunika.
No comments:
Post a Comment